Mwanaume aliyefahamika kwa Jina la Kasheshe Senkila ( Pichani ) mkazi wa Kijiji cha Shanga Kata ya Mugoma wilayani Ngara Mkoani Kagera amesalimisha Risasi 157 kwa Jeshi la Polisi wilayani humo baada ya kuzikuta kwenye kidumu cha Lita 5 alichodai kukinunua kikiwa na mafuta ya Mawese eneo la Stand ya Nyakanazi,wilayani Biharamulo.Akizungumza na Radio Kwizera leo Februari 14,2015,Nyumbani kwake, Bw Kasheshe amesema risasi hizo amezigundua jana Februari 13,2015 majira ya saa moja na nusu usiku wakati mke wake Bi Robina Senkila akipika mboga na kwamba amebaini hayo baada ya kumimina mafuta na kukuta vyuma vikiingia kwenye sufuri.

Risasi 157 zikiwa zimemiminwa kwenye Ungo kabla ya kusalimishwakuzipeleka Kituo cha Polisi Mugoma kwa ajili ya taratibu nyingine za Kiusalama

Amesema baada ya hali hiyo walitoa taarifa kwenye vyombo vya usalama wilayani Ngara kabla ya kuiarifu Radio Kwizera ikiwa ni hatua mojawapo ya kuimarisha dhana ya Polisi jamii wilayani humo.

Radio Kwizera imefika eneo la tukio na kuthibitisha Risasi 157 zilizokuwa zimemiminwa kwenye Ungo kabla ya Bw Kasheshe kuridhia kuzipeleka Kituo cha Polisi Mugoma kwa ajili ya taratibu nyingine za Kiusalama ambazo zinaendelea katika Jeshi la Polisi wilayani Ngara,mkoani Kagera.

Source:-Radio Kwizera FM.
 
 
 
Top