Rais wa Tanzania ,Dr.Jakaya Kikwete amesema amesikitishwa na kushangazwa kwa kitendo cha baadhi ya Viongozi wa dini kutoa matamko kwa waumini wao ya kuwataka kupiga kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa na kuongeza kuwa hakuwahi kudhani wala kufikiri kuwa kwa viongozi aliowaheshimu kama wangeweza Kufanya jambo kama hilo kwa waumini wao.
Mh.Kikwete ameyasema hayo jana March 28,2015, alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini kupitia kamati ya amani ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesema kitendo walichofanya viongozi hao wa dini kingeweza kuwa na tija kama katiba inayopendekezwa ingekuwa inawanyima uhuru wa kuabudu.


Na kuhusu Mahakama ya Kadhi, Mh.Kikwete amesema Serikali haitaanzisha ila waislamu wenyewe wana uhuru wa kuwa nayo ama la.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Said Meck Sadick amesema uwepo wa hali ya utulivu hasa katika mkoa wa Dar es Saam imewezekana kutokana na viongozi wa Dini kuwa naumoja ambao kila mara wamekuwa mstari wa mbele kusaidia amani idumu nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alihadi Mussa Salum amesema mkutano huo unalengo la kujadili mambo makubwa yanayolihusu taifa ambapo makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo askofu Valentino Mokiwa amesema bado ipo changamoto ya matumizi ya Demokrasia iliyopo nchini.

 
Top