Baadhi ya mashuhuda wakielekea eneo la tukio

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Shedrack Misago Ndironkeye(78) mkazi wa kitongoji cha Mkagobero kijiji cha kabanga wilayani Ngara mkoani kagera alikutwa ameuwawa kikatili  kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na baadhi ya sehemu za mwili wake kukatwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana kisha  mwili wake kuutelekezwa kichakani huku kichwa kikiwa kimepondwa vibaya na kuwekewa kokoto.

Mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa porini
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi ya tarehe 26/03/2015, ambapo inadaiwa marehemu alikumbwa na mauti hayo akitokea kilabuni kuelekea nyumbani kwake majira ya usiku wa saa mbili nakuendelea. Kamanda wa polisi kituo cha Kabanga OCS Benard Joseph alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo jeshi la polisi linawasaka waliohusika na tukio hilo maana mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kwa kuhusika na mauaji hayo.
Mwili wa marehemu ukiwa umetelekezwa porini


 
Top