Basi la Unique Express baada ya kuinuliwa na kuondoa miili ya watu watatu waliokuwa wamenasa kwenye basi.
Watu kumi wamepoteza maisha leo April 22, 2015 katika ajali iliyotokea katika kijiji cha ibingo kata ya Samuye mkoani shinyanga ajali iliyohusisha basi la UNIQUE lenye namba T 148 BKK na LORI la kampuni ya COCA COLA lenya namba za usajili T 207 BSA liliokua linakokota tela namba T 655 AJT.

Kwa maelezo ya abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Kevin Moshi ameeleza Dereva wa gari hilo alikua anaendesha kwa mwendo kasi na walipofika katika eneo la Samuye wakakutana na Lori hilo likiwa katikati ya barabara na ndipo ajali ikatokea.
Tela la lori la kampuni ya Coca cola lililokuwa linaelekea Shinyanga.

Naye Diwani wa Kata ya Samuye,Bw Amosi Shija amesema alishuhudia ajali hiyo baada ya kusikia kishindo kikubwa lakini basi hilo lilikua katika mwendo mkali hali iliyosababisha ajali kutokea baada Dereva wa basi kushindwa kupishana Lori hilo.

Miili ya marehemu ikiwekwa kwenye lori baada ya kutolewa kwenye basi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema watu tisa wamekufa hapo hapo na mtu mmoja amefariki wakati akipelekwa katika hospitali huku majeruhi 50 wakiwemo wanawake 13,wanaume 36 na mtoto mmoja wa kiume wanapata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga. Aidha amewataka madereva kuendesha magari kwa kuzingatia sheria za barabara ili kuepusha ajali ambazo zimekua zikigharimu maisha ya watu.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio,Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog.



 
Top