Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Bw.Zitto Kabwe amefafanua kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa….’’.. Kilometa 5802 kutoka Songea, Njombe, Iringa, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara na Simiyu. 
Siku 12, Wanachama 6753’’... Wastani wa kutembea Kilometa 484 kila siku.Wastani wa kuandikisha wanachama 563 kila siku. Hii ni awamu ya kwanza ya Ziara yetu ya kutambulisha chama chetu cha‪#‎ACTwazalendo.

Tulianza na mashujaa wa ‪#‎MajiMaji na tumemaliza na heshima kwa Mwasisi wa Taifa letu Mwalimu Nyerere tulipoenda kumsalimu pale Mwitongo, Butiama. 

Tunamshukuru sana Mola muweza wa yote kwa kuwa mbele yetu.Tunawashukuru wananchi wa mikoa yote 11 tuliyopoita na Watanzania wengine wote wanaotuunga mkono na wasio tuunga mkono. 

Demokrasia inataka mchanganyiko wa mawazo. Wananchi ndio waamuzi wa mwisho.
 
Top