Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Prisca Pinzure(40), mkazi wa kijiji cha Bulima kata ya Mwaluguru wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kunyongwa shingo chumbani kwa na mume wake baada ya kulewa pombe za kienyeji kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Mei 4 majira ya saa moja asubuhi mwaka huu.

Amesema kabla ya mauaji hayo Mei 3 mwaka huu,muda wa jioni marehemu alikuwa na mume wake Isaya Kuzenza (40), kwenye klabu za pombe za kienyeji wakinywa pombe hizo.

Kamanda Kamugisha amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo wanandoa hao, walikuwa na tabia ya kugombana kila wanapokunywa pombe hizo za kienyeji.

Tayari jeshi la polisi linamshikilia mme wa marehemu kwa uchunguzi zaidi juu ya mauaji hayo.

Na Marco Maduhu-Malunde1 blog

 
Top