Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wilayani Songea jana limezua kizaa zaa kwa wananchi kufuatia kuvamia mitaani, maofisini (serikali na binafsi) makanisani na misikitini wakiwa na silaha huku magari yao yakiranda kila kona na kuanza upekuzi kwa watu wote walokutana nao huku wakidai kuonyeshwa vitambulisho.
Aidha,indaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mjini hapo waliamua kujifungia ndani huku wengine wakisema kwamba jeshi hilo linawasaka magaidi waliovamia katika mji wa Songea kutokana na jeshi hilo kutowafahamisha wananchi nini hasa dhumuni la msako huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida huku akiwataka wakazi wa mjini songea kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida.

Naye Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao na kuongeza kuwa jeshi hilo hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda miji, maporini na mengineyo.

Chanzo: Mpekuzi blog

 
Top