Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwa katika mgomo leo kutokana na kutopata mkopo kwa wakati ambapo inapelekea kushindwa kabisa kuendesha maisha yao chuoni hapo baada ya serikali kupitia bodi ya mikopo kuwacheleweshea pesa zao.
Viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwatuliza wenzao leo baada ya mgomo wa wanachuo wa chuo cha RUCU kugoma wakishinikiza kupewa mikopo yao ili kuendesha maisha chuoni hapo.
Mkuu wa chuo kikuu ya Iringa Prof Joshua Madumulla akizungumza na wanafunzi hao baada ya kutokea mgomo chuoni hapo leo asubuhi.
Mmoja wa wanafunzi wa chuki kikuu cha Iringa akitoa malalamiko yake dhidi ya bodi ya mikopo kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Angeline Mabula leo kuhusu kucheleweshewa mikopo yao.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Mabula akizungumza na wanafunzi hao wakati wa mgomo wa wananchuo wa chuo cha RUCU leo
Ulinzi ulikuwa ni wakutosha chuoni hapo (Picha na Francis Godwin)

Jeshi la polisi mkoani Iringa limelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wanafunzi wa chuo kikuu cha Rucu baada ya kutaka kufanya maandamano na kusababisha vurugu chuoni hapo.
Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi ameeleza kuwa wanafunzi hao walitaka kufanya maandamano hayo kwa madai kuwa wamecheleweshewa mikopo yao.
Kamanda amesema kuwa wamewadhibiti wanachuo hao ili wasitoke nje ya geti la chuo kutokana na kuhofia kuvuruga amani .
Aidha kamanda ameeleza kuwa jeshi la polisi linawashikilia wanafunzi 89 na kusema kuwa kwa yoyote atakayejaribu kuvunja amani ni lazimawatamchukulia hatua kali za kisheria bila kujari chochote.
Hata hivyo wakizungumza wanachuo hao wamesema kuwa kucheleweshwa kwa mikopo hiyo kunachangia maisha yao kuwa magumu.
Wakati huo huo Jeshi la hilo linawashikilia viongozi watatu wa waendesha pikipiki kwa tuhuma za kuwafanyia fujo maafisa watatu wa mamlaka ya usafirishaji wanchi kavu na majini Sumatra.
Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi amesema kuwa maafisa hao wamefanyiwa fujo wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kawaida katika eneo la chuo cha mkwawa manispaa ya Iringa.
Kamanda amesema kuwa jeshi la polisi tayari limeshafungua jalada na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani muda wowote yatakapoletwa mashtaka.
Aidha kamanda amesema kuwa endapo matukio kama hayo hayata kemewa mapema yatachangia uvunjifu wa amani hivyo amewataka wananchi pamoja na wanahabari kushirikiana kwa pamoja katika kukemea masuala hayo.

Hata hivyo akizungumza afisa mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji wa nchi kavu na majini Sumatra mkoa wa iringa Bartel Patel amekiri kufanyiwa kwa kitendo hicho.

 
Top