Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mkoa wa Singida jioni hii ambapo aliwahutubia wananchi na kuwaeleza kuwa huu ni wakati wa kuchagua kiongozi wa kutuongoza hivyo ni vyema wananchi kupima na kuacha ushabiki.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na Mkuu wa mkoa wa Singida,Dkt.Parseko kone mara baada ya kuwasili mkoani humo na kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa wengine wa chama.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Wanachi wa Mkoa wa Singida jioni hii alipowasili katika ofisi za mkoa za CCM,na pia alipata fusra ya kuwahutubia wananchi,Ndugu Kinana na ujumbe wake wako njiani kuelekea mkoani Kagera kwa ziara ya siku 28. 
Baadhi ya wafuasi wa Chama cha CCM wakiwa wamekusanyika jioni hii wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana,alipowahutubia kwa muda mfupi nje ya ofisi za mkoa wa Singida jioni hii.














 
Top