Zoezi hilo limeanza leo katani humu ambapo wakazi wengi wa kata ya Kabanga wamejotokeza kwa wingi kujiandikisha katika vituo vya uandikishaji. japo kuna changamoto ndogo ya uandikishaji kwenda kwa spidi ndogo ukilinaganisha na idadi ya watu waliofika kujiandikisha, zoezi hilo linaenda vizuri katika vituo vyote huku hali ya usalama ikiwa shwari, wananchi, viongozi wa vyama vya siasa wanashirikiana na viongozi wa kata na uhamiaji kuwatambua wahamiajai haramu wanaotaka kujipenyeza ili waandikwe kama raia wa Tanzania.

Zoezi hilo litachukua siku saba kuanzia leo hivyo wakazi wa Kabanga wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili waandikishwe kwenye daftari hilo la wapiga kura wasije poteza haki yao ya msingi.

Aidha ikumbukwe kuwa wanaotakiwa kujiandikisha ni wale wenye umri wa miaka 18 na kuendelea pamoja na wale ambao kufikia mwezi oktoba mwaka huu watakuwa wametimiza miaka 18.






 
Top