Watu kumi wamekufa kwenye ajali ya basi la Simiyu lenye namba za usajili T.318 ABM iliyotokea July 22, 2015 maeneo ya Chalinze wilayani Chamwino mkoani hapa huku majeruhi na mashuhuda wakisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva.
Basi hilo ambalo lilikuwa likitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam ilitokea saa 12:30 jioni ambapo wakati gari likiwa kwenye mwendo mkali tairi lilipasuka na ndipo gari lilisererekea msituni na kugonga mbuyu. 

Kwa upande wa mashuhuda wa ajali hiyo, walisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi wa dereva uliyochangia kwa kiasi kikubwa gari kupoteza muelekeo na kuingia porini na kugonga mti.


Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma wakichukua vipimo kuchunguza ajali ya basi la Simiyu Express lenye namba za usajili T 318 ABM lililopata ajali katika kijiji cha Chalinze Wilaya ya Chamwino mkoani humo na kusababisha vifo vya watu 10 na majeruhi 53. Basi hilo lilikuwa likitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam.



Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Ezekiel Mpuya alithibitisha kupokea maiti nane na majeruhi 55.

Alisema maiti mbili ziliongezeka kutoka kwa majeruhi 55 ambao walikuwa kwenye matibabu.

Alisema waliokufa wakiwa hospitalini hapo ni mwanamke mjamzito, Rukia Mkupe na Mussa Kashinde.

Mbali na hao, wengine ni Elias Mibawa, Mfungo Matutu, Emmanuel Binamungu, Salum Ramadhan, Nestory Ambloz, Shimba Masungu, Maduhu Lushanga na Charles Mahushi.

Alisema hali ya majeruhi hao zinaendelea vizuri ambapo 27 wameruhusiwa, huku mmoja akipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wengine 28 wakiendelea kutibiwa hospitalini hapo.

Akizungumzia ajali hiyo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Mnyambugha alikiri kutokea kwa ajali hiyo saa 12:30 jioni.

 
Top