Hofu imetanda kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma baada ya mkimbizi mmoja toka nchini Burundi kufariki kwa ugonjwa wenye dalili zinazofanana na ugonjwa wa Ebola.
Hofu hiyo imetokana na mkimbizi Buchumi Joel kufariki baada ya kuugua kwa zaidi ya wiki moja na kuzikwa mjini Kigoma kwa kuzingatia taratibu za afya, ambapo wamesema ni muhimu serikali kudhibti raia toka nchi jirani ambao wamekuwa wakiingia bila kuzingatia au kupimwa afya zao hali ambayo ni hatari.

Akizungumzia tukio hilo, kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma, Shija Ganai ambaye pia ni afisa afya wa mkoa, amesema mkimbizi huyo alianza kuugua akiwa katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu na baadaye kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kigoma baada ya kuugua ugonjwa wenye dalili za ugonjwa huo hasa baada ya kuanza kutokwa damu katika sehemu zote za matundu ya mwili.

Ameeleza kuwa kutokana na hali yake na licha ya kwamba hawajathibitisha kama ameugua ugonjwa wa Ebola, tahadhari zote zimechukuliwa na serikali na mashirika ya afya kimataifa ili kuhakikisha ugonjwa wowote aliokuwa nao hausambai.

CHANZO: ITV
 
Top