Uchaguzi mkuu katika jimbo la Shinyanga mjini umeingia dosari baada ya wagombea wa ubunge wa upinzani Chadema na APPT Maendeleo kutoka katika ukumbi wa kuhesabu kura na kutangazia matokeo kwa madai kuwa uchaguzi huo ulikuwa umegubikwa na rushwa,vitisho na udanganyifu wa hapa na pale hali ambayo wamesema kwa vyovyote vile matokeo haya wezi kuwa halali..na sasa kinachoendelea ni kwaba kura zinahesabiwa upya kwa vituo vyote 275…Mgombea ubunge wa Ukawa/Chadema Patrobas Katambi ameondoka eneo la kutangazia matokeo na wafuasi wa Chadema.
Askari polisi wapo wa kutosha mtaani na eneo la tukio-Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde yuko eneo la tukio ametuletea picha zifuatazo….
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Shinyanga mjini Lewis Kalinjuna akizungumza kabla ya kuwakaribisha wagombea kuzungumza kabla ya zoezi la kuhesabu kura halijaanza
Wagombea na wafuasi wa vyama wakiwa katika ukumbi wa kuhesabia kura mudaa huu
Katambi akizungumzia namna uchaguzi ulivyogubikwa na rushwa na udanganyifu ambapo mgombea CCM Stephen Masele amekuwa akicheza rafu mwanzo hadi mwisho wa uchaguzi
Wananchi wakifuatilia kinachoendelea
Mgombea ubunge wa APPT Maendeleo Emiliana Tambwe akisema uchaguzi ulikuwa siyo halali
Katambi akizungumza na waandishi wa habari
Katambi akiondoka ukumbini
Wafuasi wa chadema wakiwa na mgombea wao
Wanaondoka
Katambi na wafuasi wa Chadema wakiwa katika ofisi za chadema
Ulinzi mtaani
Ulinzi eneo la tukio
Gari la maji ya kuwasha
Picha zote/ stori na Kadama Malunde-Malunde1 blog