Watu kumi na mbili wamefariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa baada ya Lori la mizigo kugongana basi la NEW FORCE leo tarehe 18/12/2015.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni ya Newforce aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF linalofanya safari za Tunduma Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba T616DEF eneo la Igeme kijiji cha Mahenge,wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa mbele kidogo ya mlima kitonga katika barabara kuu ya Dar - Mbeya baada ya Lori la mizigo kugongana na Bus hilo lililokuwa linatokea Dar kwenda Tunduma.

Bus na Lori yote yalianguka baada ya kugongana. Watu 12 yaani wanaume 8 na wanawake 4 wamepoteza maisha. Watu 28 ni majeruhi wamekimbizwa hospitali huku wengi wao wakiwa na hali mbaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo ilosababisha vifo na kujeruhi watu. Madereva wa basi na lori na hali zao siyo nzuri.