Jiwe hilo lililopigiliwa kitu kama nondo yenye umbo kama mtaimbo au msumari linapatikana eneo la Msumba kijiji cha Nyamiaga, kata ya Nyamiaga wilayani Ngara mkoani Kagera. Wenyeji wa eneo hilo wanadai jiwe hilo lina muda mrefu linakitu hicho huku wengine wakisema walizaliwa na kukua wakiliona hivyo hivyo na kitu hicho. Pia wamesema wapasua mawe walijaribu kulipasua ili wajue nini kilichomo walishindwa.
Mtandao huu umeongea na bibi mmoja ambaye kidogo ni wa zamani amesema kati ya miaka ya 1965 hadi 1970 ndio kitu hicho kiligongelewa humo na wazungu waliofika eneo hilo na kupigilia kitu hicho, watu wengi waliamini kuwa ni alama ya wazungu waliweka huku wengine wakidai alama hiyo ni ishara ya kuwepo kwa madini ndani ya ardhi ya eneo hilo.

Kwa watakaopenda kwenda kushuhudia kama mimi ukitoka Ngara kuelekea Murukulazo ukifika Msumba center kuelekea Murukulazo kabla hujafika mbali kuna kidaraja sasa kabla hujakifikia hicho kidaraja mkono wa kulia jiwe hilo lipo hapo.

Kama una kitu cha maajabu wilayani Ngara tutumie picha na habari kwenye WhatsApp No. +255766378713
 
Top