Mfanyabiashara Andrew Gatawa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuharibu miundo mbinu ya reli.
Gatawa amehukumiwa kifungo hicho katika mahakama ya Ilala baada ya kupatikana na hatia ya kung’oa mataruma ya reli ambayo ni mali ya Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA)
Mahakama imewaachia huru washitakiwa wawili ambao walikuwemo katika kesi hiyo kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao hivyo kushindwa kuwatia hatiani .
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Flora Mujaya amewataja washtakiwa walioachiwa huru na mahakama kuwa ni Issa Seif na Abdallah Hamidu kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka hivyo kushindwa kuwatia hatiani.
