Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine 18 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Taqbiir kugongana na lori la mafuta mkoani Singida. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi,Thobias Sedoyeka amethibitisha , kutokea kwa ajali hiyo na kusema basi lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Katoro mkoani Geita. 

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 usiku jana katika eneo Kizonzo Wilaya ya Iramba mkoani Singida ma ilihusisha basi aina ya Scania lenye namba za usajili T230 BRJ lililokuwa likiendeshwa na Charles Kikaena lililogongana na lori la mafuta T793 CBH lililokuwa na tela T273CBH lilokuwa likiendeshwa na dereva Mohamed Rajabu. 

Chanzo cha ajali ni dereva wa basi aliyekuwa akilipita lori mali ya kampuni ya Coca Cola T314CTS lililokuwa na tela T196 BEF na kugongana na lori la mafuta na kisha lori hilo kulichana basi kuanzia mbele upande wa dereva hadi mwisho na kusababisha vifo hivyo vya watu 12 na majeruhi 18 na basi hilo lilikuwa na abiria 51. 

Miongoni mwa waliokufa wanaume ni saba akiwemo mtoto mdogo mmoja na wanawake watano kati yao watoto wawili. Majeruhi wa ajali hiyo walifikishwa katika Hospitali ya serikali ya Kiomboi mkoani Singida kwa matibabu. 
Na Father Kidevu Blog
 
Top