Ni muonekano wa Lori la Mizigo katika barabara ya Nyakanazi-Ngara eneo la mteremko mkali wa Nyabugombe mpakani mwa Wilaya ya Ngara na Biharamulo mkoani Kagera,ambalo lilipata ajali ya tela lake kung'oka na kukwama katikati ya barabara hiyo na kuleta shida ya magari kupita kama picha zinavyoonesha hapa chini.
.........Hili ndilo tela lililong'oka na kujikita chini ,hali iliyoleta ugumu wa magari yanayopanda mlima huo na kuteremka kupata ugumu kupita,kwa sasa limeondolewa .changamoto imebaki katika ubovu wa eneo hilo kujaa mashimo.
Fuso hili lilianguka pembezoni mwa barabara ya Nyakanazi-Ngara eneo la mteremko mkali wa Nyabugombe ,baada kufeli kupanda mlima na kurudi nyuma,hakuna aliepoteza maisha katika ajali hiyo.
CREDIT: mwanawamakonda.blogspot.com





