Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuanzisha mahakama ya mafisadi.
Akisoma hotuba ya bajeti hiyo bungeni mjini Dodoma, Dk Mpango amesema mbali na fedha hizo, Serikali pia imetenga Sh72.3 bilioni kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili kuiwekezesha taasisi hiyo kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Amesema bajeti hiyo inalenga kutatua kero katika maeneo yaliyolalamikiwa na wananchi likiwemo suala la rushwa na ufisadi.
Mahakama hiyo ni ahadi Rais John Magufuli akaibeba kwenye kampeni zake wakati Taifa likipigia kelele ufisadi uliokithiri nchini.

Aprili 22 mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi yake, alisema Serikali imeanzisha Divisheni ya Rushwa na Ufisadi ya Mahakama Kuu itakayoanza kufanya kazi Julai mwaka huu na itaanza kwa kushughulikia kesi 10 ambazo ucnhunguzi wake umekamilika





 
Top