Maisha ya kiungo wa Mancheter United, Michael Carrick yataendelea kuwepo katika klabu hiyo baada ya kocha mpya wa klabu hiyo ambaye amechukua nafasi ya Louis Van Gaal, Jose Mourinho kumwongezea mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia klabu hhiyo.
Carrick ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika amepata nafasi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo baada ya kocha Mourinho kumwambia kuwa anahitaji kufanya nae kazi na hivyo kupewa mkataba wa mwaka mmoja ambao utamalizika mwakani.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali za michezo zimeeleza kuwa Carrick aliongezewa mkataba siku ya Jumanne.
 
Top