Mwenge wa uhuru uliingia wilayani Ngara ukitokea mkoa wa Kigoma ambapo tarehe 23/07/2016 ulipokelewa eneo la Murusagamba wilayani Ngara na kuzungushwa wilayani humo kukagua miradi na kuzindua miradi mipya tisa yenye thamani ya billion 1.9. Mwenge huo ulipokelewa na kukesha katika mji mdogo wa Kabanga wilayani Ngara ambapo mwitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa. Amani ilitawala tangu kupokelewa kwa mwenge huo hadi asubuhi baada ya mkesha kila mmoja aliondoka uwanjani salama.
























 
Top