Bingwa wa Soka mkoa wa Kagera ,Kumuyange FC.

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) imeendelea tena May 7,2018 kwenye vituo vinne.
Ligi hiyo itashirikisha timu 28 zilizogawanywa kwenye makundi manne kwenye vituo vya Geita, Singida, Rukwa na Kilimanjaro na kila kundi likiwa na timu saba (7)

ambapo mbili zitakazofanya vyema zitapanda ligi daraja la pili wakati zitakazobaki zitarudi ligi ya mkoa.

Katika kituo cha Geita,uwanja wa WAJA -Mabingwa wa Soka mkoa wa Kagera, Kumuyange FC wameanza kwa kishindo kikubwa cha ushindi wa bao 6-2 dhidi ya Zimamoto FC ambao ni Mabingwa wa Soka mkoa wa Shinyanga.

Magoli ya Kumuyange FC yalifungwa kwa Hat trick mbili za Mchezaji Ezra na Ibra.
 
Top