Diamond
kuwania tuzo za BET (BET Awards 2014)
Msanii kutoka
Tanzania, Diamond Platnumz ameipa tena heshima kubwa bendera ya nchi yake kwa
kuingia kwenye kipengele cha msanii bora wa Kimataifa (Best International Act).
Hii ni hatua kubwa kwa Diamond baada ya siku chache tu nyuma kutangazwa kuingia
kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards).
Diamond Platnumz
kwenye kipengele hiki cha tuzo kubwa za televisheni ya burudani BET ya
Marekani, yupo kama Best International Act Africa na anawania tuzo hii na
wasanii kama Davido kutoka Nigeria, Mafikizolo kutoka Afrika Kusini, Tiwa
Savage kutoka Nigeria, Toofan na Sarkodie wa Ghana.
BET imetumia twitter kutoa hii taarifa
kuthibitisha tiki kwa Diamond na kuumpa hongera kama msanii pekee kutoka Afrika
Mashariki. Hongera mwana, Diamond Platnumz!!