Hasira: Jose Mourinho alimlaumu mwamuzi kwa kuwaharibia maandalizi ya msimu.MBWATUKAJI Jose Mourinho amemlaumu mwamuzi kwa kusababisha
maandalizi ya msimu ya Chelsea kuwa shubiri baada ya kutandikwa mabao 3-0 na Werder Bremen.
Didier Drogba akicheza kwa mara ya kwanza tangu arejee Chelsea, alishindwa kung`ara jana na kushuhudia vijana hao wa darajani wakiangukia pua.
Mwamuzi Harm Osmers, kutoka Hannover aliwapa penalti mbili rahisi wenyeji, moja ni baada ya John Terry kuushika mpira kwa mkono na nyingine kuangushwa kwa Nathan Ake.
Maamuzi hayo ya penalti hayakumridhisha Mourinho na kuyaita 'hayana maana'.
Baada ya kupoteza mechi katika ziara hiyo nchini Ujerumani, Mourinho na Chelsea yake wamerejea usiku mjini London.
Hahahaha! hapa hakuna kitu! Mouringo alipigwa picha akicheka baada ya maamuzi ya penalti
John Terry aliushika mpira kwa mkono kwenye eneo la hatari na kusababisha penalti, lakini Mouringo amesema maamuzi hayo hayana maana.
"Sijajifunza lolote kutoka kwenye mchezo,' Alisema Mourinho. 'Matarajio yetu hayajatimia kwasababu tulipoamua kuwa na mechi hii mjini Bremen tulitegemea changamoto nzuri.
'Tuligemea mchezo wa kasi na ushindani, lakini tulipokuja hapa, mwamuzi alidhani mchezo huu ni muhimu kwa mashabiki wa Bremen ili wafurahi na aliua mechi.
'Mchezo huu ungekuwa mzuri kwetu. Nimeipenda timu ya Werder Bremen-wana kasi, nguvu na wanalinda na watu wengi. Upinzani ni wa kutosha, lakini tungeweza kucheza vizuri.'
Mshambuliaji Didier Drogba hakuonesha makali katika mechi ya jana.