Tabasamu bab kubwa: Mario Balotelli (kushoto, akiwa na Mamadou Sakho) hawataungana Liverpool mwezi huu.KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amekanusha
tetesi za kutaka kumsajili mshambuliaji wa AC Milan, 'Mtukutu' Mario Balotelli.
Rodgers alihusishwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City baada ya kumzungumzia Balotelli wakati maandalizi ya mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya AC Milan.
Liverpool wapo sokoni kutafuta mshambuliaji baada ya dili la kumsajili Loic Remy kushindikana, lakini Rodgers amekanusha kuitaka saini ya Balotelli.


Uvumi! Brendan Rodgers alisema Balotelli hatajiunga Anfield


Tuli tuli! Jordan Ibe akivuta bukuta ya Balotelli katika ushindi wa Liverpool wa mabao 2-0 dhidi ya AC Milan.


Amesepa: Luis Suarez aliondoka klabuni mapema majira ya kiangazi akienda kutafuta makombe Hispania.
Wakati anazungumzia mechi ya fainali ya kombe la kimataifa dhidi ya Manchester United leo jumatatu, Rodgers alisema: "Kiukweli nawaambieni kwamba hatajiunga Anfield.
'Niliulizwa swali kuhusu Balotelli na nilizungumzia jinsi alivyo na kipaji na jinsi alivyo mchezaji mzuri.
'Ni mchezaji wa ajabu, lakini ni mchezaji wa AC Milan, nilitoa tu maoni yangu, lakini haimaanishi nitamsajili.'
Rodgers alisema Man United inaweza kuibuka tena katika ligi kuu England msimu ujao chini ya kocha mpya Louis Van Gaal baada ya kumaliza nafasi ya 7 wakati wa kocha David Moyes.
Alitabiri mechi ya ushindani baina ya timu mbili hasimu itakayopigwa leo mjini Miami, lakini alisisitiza kuwa haitakuwa na maana kubwa na kutabiri mbio za ubingwa England.








 
Top