Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Kibimba Bw.John Shimilimana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kilichofanyika Agost 05,2014,katika ukumbi wa Halmshauri hiyo Habari/Picha Na:-Shaaban Ndyamukama-Ngara.



Kulia ni Diwani wa Kata ya Kabanga Bw.Soud Said akifatilia kile kilichokuwa kinaendelea wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kilichofanyika Agost 05,2014.




Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ngara,Bw.Deogratius Ntukamazina akinukuu baadhi ya mambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kilichofanyika Agost 05,2014,katika ukumbi wa Halmshauri hiyo .


Picha juu na chini ni Madiwani wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kilichofanyika Agost 05,2014,katika ukumbi wa Halmshauri hiyo .




Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani kagera jana limetangaza kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw. Colnery Ngudungi kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya kumchukulia hatua aliyekuwa Meneja wa Mamlaka ya maji mjini Ngara Bw.Edward Magai kwa kufuja fedha zaidi ya Sh 32 milioni.


Wakichangia hoja ya ubadhilifu wa fedha alizotoa Rais kikwete kwa mamlaka ya mji mdogo wa Ngara kiasi cha Sh 200 milion huku kiasi kilichokwisha pokelewa ni Sh 150 milioni ,ambapo Madiwani hao wameonesha kusikitisha na utekelezaji wake kusuasua huku hakuna juhudi zinazoonekana katika matumizi ya fedha hizo.


Diwani wa Kata Mulukulazo,Bw. Mukiza Byamungu amesema atafungua kesi mahakamani dhidi ya viongozi wa halmashauri hiyo kwa kuendelea kumkumbatia meneja huyo ambaye amefuja fedha hizo na ameshastaafu.


Naye Diwani wa Kata ya Ntobeye Bw.John Ruzige amesema Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa namna moja ama nyingine anahusika na kupotea kwa fedha hizo kwani kila kunapokuwa na kikao chenye hoja za maji na changamoto za halmashauri hukwepa kikao nakukaimisha mkuu wa idara.


Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi, mfanyakazi anapoacha ma kustaafu kiutumishi anastahili kukabidhi nyaraka mbali mbali lakini Bw.Edward Magai hajakabidhi mali za halmashauri wala nyaraka za serikali.


Amesema fedha kutoka ofisi ya Rais ni kiasi cha jumla ya Sh 150 milioni na kati ya fedha hizo Sh 37 milioni zimetumika kununua vipuli vipya vya kufunga mitambo ya kusukuma maji na kiasi kingine kilichobaki hakikufanya jambo lililokusudiwa la kuwapatia wananchi huduma ya maji .





Aidha Diwani wa Mamlaka ya mji ndogo wa Ngara,Bw. Charles Rujuba amesema kuna haja ya kuitisha kikao cha baraza la dharula ndani ya siku saba kutaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutoa maelezo juu ya suala hilo.


“Katika mamlaka ya maji mjini ngara meneja aliyeshika nafasi hiyo hana vitendea kazi kwa kuwa kabati zimefungwa na meneja aliyestaafu Magai amejimilikisha funguo na kukwamisha shughuli za kijamii”Alisema Rujuba.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Bw Herman Hume amesema Meneja huyo alipewa siku 10 kujieleza kuhusu matumizi ya fedha hizo lakini hakutekeleza hivyo anaridhia maoni ya baraza na atahakikisha mtuhumiwa anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria



Katika baraza hilo madiwani wamemchagua kwa mara nyingine aliyekuwa makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ,Bw. Soud Mkubila ambaye ataongoza halmashauri ikiwa ni kipindi chake kwa mara ya nne.


Wajumbe wengine wa kamati waliochaguliwa ni Mwenyekiti kamati ya Elimu,Afya, na Maji (Willibard Bambara), Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira ( John Ruzige) na kamati ya Maadili ya wilaya ni Bw. Tomson Seyongwe.


 
Top