Chama cha Demokrasia na maendeleo mkoani Arusha kimeliweka jeshi la polisi katika wakati mgumu wa kudhibiti maeneo yote ya jiji hilo na viunga vyake ukiwemo uwanja maarufu wa mikutano wa chama hicho wa Samunge kufuatia kuwepo kwa taarifa za wanachama wa chama hicho kutaka kuunga mkono maandamano yasiyokuwa na kikomo ya kupinga vikao vya bunge maalum la katiba vinavyoendelea.
Akizungumza na vyombo vya habari, mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha Bw Amani Golugwa amesema anashangazwa na hatua ya polisi ya kusambaza askari wake kila kona kudhibiti maandamano hayo kabla ya chama hicho kuanza maandamano hatua ambayo amezidi kusisitiza kuwa ni ushindi wa Chadema kwani hawakuwa na agenda ya kundamana bali walikuwa na machakato wa maandalizi ya maandamano hayo yasiyokuwa na kikomo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la jiji la Arusha Bw Godbles Lema aliyeonekana kuwa karibu na kikundi cha polisi hao waliokuwa doria amesema amemuamua kukaa karibu na kikundi cha askari wa kutuliza ghasia kumlinda na pia kuepusha kile kinachodaiwa kama muwaandaji wa maandamano hayo na kusisitiza kuwa bado azma ya kufanyika kwa maandamano hayo ipo kwani wamebuni mbinu mpya ya kuwasilisha ujumbe wao maandmano hayo yakiwemo ya polisi kudhibiti maeneo yote ya jiji hilo.
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoani Arusha Bw Liberatus Sabas akizungumza kwa ufupi kwa njia ya simu amekanusha kudai kuwepo kwa askari hao ni sehemu ya ulinzi na ndo maana hakuna mtu yeyote aliyekamatwa, huku baadhi ya wananchi wakiitaka serikali kuruhusu maandamano hayo kwa amani.
chanzo:ITV