MWENYEKITI WA CHADEMA KAHAMA JUMA PROTAS.
Wakati jeshi la Polisi Nchini likipinga maandamano yoyote, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilayani Kahama mkoani Shinyanga Kimetangaza kufanya maandamano ya amani kupinga kuendelea kwa bunge la Katiba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani Humo Juma Protas amesema maandamano hayo yatafanyika kesho mwaka huu kuanzia asubuhi kwa kushirikisha wanachana na wananchi wengine wanaounga mkono jambo hilo. 

Protas amesema maandamano hayo yataanzia katika ofisi ya Chama hicho, na watazunguka katika mitaa mbalimbali ya mji wa Kahama na kuhitimisha kwa mkuu wa wilaya ya Kahama na kwamba lengo kuu ni kuitaka serikali kusitisha bunge la katiba. 

Amesema katiba Mpya kwa vyovyote haiwezi kupatikana kwa mwaka huu hivyo kuendelea kwa bunge la katiba ni kutumia vibaya fedha za wananchi na kwamba wanatumia sheria ya maandamano ya kimataifa kwa kufunga kitambaa cheupe mkononi kuashiria amani. 

Protas amesema kwa upande wa Halmashauri ya Msalala, chama hicho kitafanya maandamano siku hiyohiyo kuanzia ofisi za Chadema-Segese na kuzunguka Mitaani na kuhitimisha katika uwanja wa shule ya msingi Segese kwa kuzungumza na wananchi. 

Hata hivyo amesema licha ya kuomba Kibali kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama, hakuna majibu waliyopewa na jeshi hilo, huku mwenyekiti huyo akisisitiza watatumia kuwa sheria ya kimataifa kufanya maandamano bila kuathiri kitu chochote.

CHANZO: FARAJI MFINANGA
 
Top