Vinara wa Ligi Kuu Uingereza 2014/2015- Chelsea Leo September 27, 2014,wakicheza kwao Stamford Bridge wameitandika Aston Villa Bao 3-0 na kuzidi kupaa kileleni kwa kufikisha Pointi 16 sasa.
Hadi Mapumziko Chelsea walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Oscar la Dakika ya 7 huku Dakika ya 59 Diego Costa aliipa Chelsea Bao la Pili kwa Kichwa na Willian aliipa Chelsea Bao la 3 katika Dakika ya 79 baada ya Shuti la Diego Costa kuokolewa na Kipa Guzan na kumkuta Willian.


Aidha Bao la Dakika ya 91 la Sentahafu Phil Jagielka likawapa Everton Sare ya Bao 1-1 walipocheza Mechi ya Merseyside Uwanjani Anfield na Watani zao Liverpool katika mchezo wa Ligi kuu Uingereza 2014/2015 leo Septemba 27,2014.


Liverpool walifunga Bao lao katika Dakika ya 65 kwa Shuti safi la Nahodha wao Steven Gerrard.

Huku Anfield ikisheherekea ushindi dhidi ya Mahasimu wao na Dakika zikiyoyoma Krosi ya Aiden McGeady iliokolewa kwa Kichwa na Mpira kumkuta Phil Jagielka na kufumua Shuti safi sana kutoka Mita 30 na kufanya Gemu imalizike 1-1.


Wakicheza kwao Old Trafford, Manchester United wameifunga West Ham Bao 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kukwea hadi Nafasi ya 7 lakini watamkosa Nahodha wao Wayne Rooney kwa Mechi 3 zijazo baada ya kutwangwa Kadi Nyekundu.

Hadi Mapumziko Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao za Nahodha Wayne Rooney, ambae sasa ametimiza Miaka 10 akiwa Old Trafford, baada kuunganisha pande safi la Rafael katika Dakika ya 5 na Robin van Persie kupiga Bao la Pili katika Dakika ya 22 baada ya kazi njema ya Ander Herrera na Radamel Falcao.

West Ham walifunga Goli lao baada ya kutokea kizaazaa kufuatia Kona na Diafra Salho kukwamisha Mpira wavuni katika Dakika ya 37.


Dakika ya 54 Man United walibakia Mtu 10 baada ya Refa Lee Mason kumpa Kadi Nyekundu Nahodha Wayne Rooney kwa madai amemchezea Rafu mbaya Stewart Downing.

Hii inamaanisha Rooney atazikosa Mechi 3 za Timu yake dhidi ya Everton,West Brom na Chelsea.



Zabaleta kulia akimpongeza lampard baada ya kufunga bao la nne ,ambapo Mabingwa watetezi Manchester City imeshinda mabao 4-2 dhidi ya wenyeji Hull City katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Uingereza jioni ya leo September 27, 2014.

Mabao ya City yamefungwa na Sergio Aguero dakika ya saba, Edin Dzeko dakika ya 11 na 68 na Frank Lampard dakika ya 87, wakati mabao ya Hull yamefungwa na Eliaquim Mangala aliyejifunga dakika ya 21 na Hernandez kwa penalti dakika ya 32.


As It Stands Tables EPL 2014/2015.
 
Top