Upande wa kushoto ni wachezaji wa timu ya mkoa wa Muyinga



wachezaji wa timu ya Kabanga Fc

 Timu ya Kabanga ikikabidhiwa mpira mpya kutoka kampuni ya Be Forward JP

Mchezo huo ilichezwa jana tarehe 21/09/2014 katika uwanja wa Kabanga Ngara Mkoani Kagera ukiwakutanisha na timu ya Mkoa wa Muyinga ya nchini Burundi. Mchezo huo ulikuwa wa uzinduzi wa udhamini wa kampuni inayouza magari duniani ya Be forward JP ya nchini Japan ambapo imetoa udhamini kwa timu ya Muyinga kwa upande wa Burundi na kwa upande wa Tanzania wametoa udhamini wao kwa timu ya kabanga fc ya wilayani Ngara mkoani Kagera.
Katika mchezo huo uliowavutia mashabiki, timu ya mkoa wa Muyinga iliibuka na ushindi wa gori 4 kwa 2 dhidi ya wenyeji wa Kabanga, aidha kipindi cha kwanza kilimalizika huku timu zote zikiwa bado hazijaona lango na katika kipindi cha pili timu ya wenyeji ndo ilikuwa ya kwanza kupata gori kupitia kwa Mwalimu Moses aliyepiga shuti kali na lililojaa wavuni baadae kidogo timu ya Muyinga ilisawazisha gori hilo kupitia kwa mshambuliaji wao Javier na hivyo kuwapa nguvu iliyowapelekea kuongeza gori la pili hadi la nne lakini wachezaji wa timu ya Kabanga walishtuka na kupata gori la pili hivyo kulingana na muda hawakuweza kurudisha magori yote manne. Hadi kipenga cha mwisho kikipulizwa na mwamuzi wa mchezo huo Mwalimu Jasson Meshaki matokeo yalisomeka Muyinga 4 na Kabanga 2.
Akiongea kocha wa timu ya Kabanga ambaye pia ni mchezaji Ndugu Ezra Essau amekiri kuwa sababu kubwa ya kufungwa ni kutokuwa na mazoezi kwa timu yake ambapo wachezaji wanazembea kuja mazoezini na hata havyo waliruhusu mechi hiyo sababu ya huo uzinduzi wa kampuni ya Be forward la sivyo wasingeita mechi maana hali ya timu yake ki mazoezi bado si nzuri zaidi amewaomba wachezaji kujitokeza kwenye mazoezi ili kuimarisha timu maana ni aibu kubwa timu kudhamini na kampuni kubwa na kuendelea kufungwa na kutojitokeza mazoezini.
 
Top