Serikali inatarajia kuanza kutumia technolojia mpya ya kudhibiti ajali za barabarani ikiwemo ya kufunga vifaa maalumu vya kurekodi makosa yanayofanywa na madereva hatua ambayo licha ya kuwezesha kuodoa malumbano kati yao na askari itaziba mianya ya rushwa.
Akizungumza katika kilele cha wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyokuwa inafanyika Arusha naibu waziri wa mambo ya ndani Mh Pireira Selima amesema taratibu za kuanza kutumika kwa mfumo huo zimeshaanza na utatekelezwa kwa awamu na kwa kuzingatia vipoaumbele kulingana na uwezo wa bajeti.

Akifunga maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Manyara Mh Erasto John Mbwiro amelitaka baraza la taifa usalama barabarani kupanua mtandao wa kuweka utaratibu utakaowawezesha wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwajibika zaidi katika kudhibiti ajali badala ya kuwabana maderva pekee ambao asilimia kubwa wamekuwa wakifuata maelekezo ya wenye magari.

Aidha mbwa mwiro pia amelitaka baraza hilo kuangalia uwezekano wa kujenga hoja itakayowezesha kuboresha maslahi ya askari wa usalama barabarani kama hatua ya kuwaepusha na vishawishi vya rushwa.

Awali mkuu wa kikosi cha usalama barabaani nchini kamanda Mohamedi Mpinga amesema mambo yote yalifanyika katika kipindi chote cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yatakuwa yanaendelea hasa kutoa elimu na ameendelea kuwataka wadau wote kila mmoja kuona umuhimu wa kutimiza wajibu wake.
 
Top