Mazishi ya waliokuwa wanafunziwa shule ya sekondari Uhuru Hussein Alley na Kaseja Stanley waliofariki dunia wakiogelea kwenye bwawa la Ning'wa lililoko nje kidogo ya mji wa Shinyanga yamefanyika jioni hii.Hussein Alley amezikwa katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga huku Kaseja Stanley akizikwa katika makaburi ya Lubaga.Pichani ni watu wenye mapenzi mema wakiwa wamebeba mwili wa Hussein Alley kutoka nyumbani kwao Majengo kupeleka kwenye msikiti wa Majengo kabla ya kuupeleka kwenye makaburi ya Nguzo nane jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde
Kulia ni kijana Hussein Alley aliyekuwa anasoma kidato cha pili katika shule ya Uhuru sekondari mjini Shinyanga enzi za uhai wake.Malunde1 blog haijafanikiwa kupata picha ya mwanafunzi wa pili Kaseja Stanley.Kwa maana hiyo aliyeko kwenye picha kushoto(mrefu) hahusiki katika tukio hilo(siyo Kaseja Stanley)-Picha na Kadama Malunde

 
Katikati ni Hussein Alley enzi za uhai wake akiwa na wadogo zake(Alley Shaban kulia kwake na kushoto ni Mudy Mohamed_ picha hii imepigwa juzi siku ya sikukuu ya Idd. Kifo cha Hussein kinazua maswali mengi kwani inaelezwa kuwa hakuwa na mazoea ya kwenda kwenye bwawa hilo na kwamba hata baada ya kutolewa ndani ya bwawa hilo hakuwa amekunywa maji,lakini mwenzake Kaseja tumbo lilikuwa limejaa maji.-Picha na Kadama Malunde

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwao na Hussein Alley( kwa mzee Alley mtaa wa Majengo mjini Shinyanga.Mamia ya watu wakiwemo walimu,wanafunzi,waandishi wa habari,viongozi wa dini na siasa wamehudhuria mazishi ya wanafunzi hao-Picha na Kadama Malunde

Nyumbani kwa mzee Alley vilio, nyuso za uhuni zilitawala.Wanafunzi hao wawili waliokuwa wanasoma katika shule ya sekondari Uhuru mjini Shinyanga wamefariki dunia wakati wakiogelea kwenye Bwawa la Ning'wa lililopo nje kidogo ya mji wa Shinyanga.-Picha na Kadama Malunde

Kwa mujibu wa kaka wa mmoja wa wanafunzi hao Shabaan Alley ambaye ni mwandishi wa Star tv/Rfa aliyezungumza na malunde1 blog amesema mdogo wake na mwenzake hawakuonekana nyumbani tangu juzi jioni baada ya kutoka shuleni na waligundulika wakiwa wamefariki dunia katika bwawa la Ning'wa jana jioni saa 11.

Nguo zao na baiskeli waliyokuwa nayo vilionekana pembezoni mwa bwawa hilo ndipo wakagundulika kufa maji katika bwawa hilo leo jioni majira ya saa 11.-Picha na Kadama Malunde

Wakazi wa Shinyanga wakisindikiza mwili wa marehemu Hussein Alley kwenda katika nyumba yake ya milele jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde

Mazishi ya kijana Hussein Alley yamehudhuriwa pia na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Khamis Mgeja(mwenye kibaragashia) na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago (kulia kwake na Mgeja)-Picha na Kadama Malunde

Mwili wa marehemu Hussein Alley ukifikishwa kwenye makaburi ya Nguzo nane jioni hii kwa ajili ya mazishi-Picha na Kadama Malunde
 Mazishi yanaendelea-Picha na Kadama Malunde

Mazishi yanaendelea...pichani ni vumbi la udongo-Picha na Kadama Malunde

Shekhe wa manispaa ya Shinyanga Balilusa Khamis akizungumza baada ya shughuli ya mazishi ya Hussein Alley katika makaburi ya Nguzo nane ambapo aliwaasa wananchi kuwa na heshima wanapokuwa katika maeneo ya makaburini wakati shughuli za mazishi zikiendelea kwani kuna baadhi ya watu wakifika hapo kazi yao ni kuongea na simu,kuongea badala ya kuwaombea marehemu-Picha na Kadama Malunde

Kaka yake na Hussein Alley,Shaban Alley(wa tatu kutoka kushoto) akiwa eneo la mazishi leo -Picha na Kadama Malunde

Katikati ni shekhe wa wilaya ya Kahama Omary Adam Damka akitoa mawaidha baada ya mazishi ya kijana Hussein ambapo aliwataka wanadamu kujiandaa na kifo kwa kutenda mambo mema kwani hakuna ajuaye siku ya kufa kwake-Picha na Kadama Malunde
Baada ya mazishi ndugu wa marehemu Hussein wakiwa kwenye kaburi(mwenye kanzu ni ndugu Shaaban Alley kaka yake na Hussein Alley)-Picha na Kadama Malunde
 
Top