Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Mohamed Mpinga pamoja na Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga na mafisa wa TBL wakifurahia baada ya kujionea namna zoezi la upimaji wa afya kwa madereva katika eneo la Makuyuni wilayani Monduli lililovyofanikiwa wakati wa wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani lililofanyika kitaifa mkoani Arusha.
Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Dar es Salaam Dk. Charles Msenga akizungumzia juu ya mafanikio waliyopata wakati wa zoezi la kupima afya za madereva takribani 800 mkoani Arusha, katika eneo la Makuyuni wilayani Monduli, pembeni yake ni Mkuu wa wilaya hiyo Jowika Kasunga.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akizungumza mara baada ya kutembelea mabanda na kujionea jinsi zoezi la upimaji afya kwa madereva lilivyokuwa likifanyika wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani, ambapo zoezi hilo lilifanyika katika eneo la Makyuni wilayani Monduli. Pembeni yake mwenye kofia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Mohamed Mpiga na Meneja wa Mauzo Kanda ya Kaskazini Davis Degratius.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga akizungumzia juu ya mafanikio ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofadahiliwa na Kampuni ya BIA TBL wakati wa zoezi la upimaji wa afya kwa madereva lililofanyika Makyuni wilayani Monduli, Arusha kulia kwake ni Meneja wa Kiwanda cha Arusha Salvatory Rweyemamu na kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha ... Mwakyoma akiunga mkono zoezi la upimaji wa afya kwa madereva wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani lililofanyika Makuyuni, wilayani Monduli mkoani Arusha kwa kutoa damu kwa ajili ya kupima vipimo vya sukari mwilini.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Marrison Mwakyoma akipima macho yake kama sehemu ya kuhamasisha upimaji wa fya kwa madereva wa mabasi na magari ya mizigo wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani zoezi hilo lilifanyika eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Marrison Mwakyoma akipima macho yake kama sehemu ya kuhamasisha upimaji wa fya kwa madereva wa mabasi na magari ya mizigo wakati wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani zoezi hilo lilifanyika eneo la Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akisisitia jambo wakati alipokuwa akipewa maelekezo ya namna wataalamu wanavyochukua vipimo vya afya kutoka kwa madereva wa mabasi na magari ya mizingo wakati wa zoezi la upimaji wa afya lililofanyika Makuyuni wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani