Watu wawili walioiba pikipiki tatu na kumjeruhi kwa nondo fundi pikipiki mmoja baada ya kumuibia moja kati ya pikipiki hizo wameuawa na wananchi katika maeneo ya Mahiro kata ya Matogoro Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma huku waendesha Bodaboda wakipongeza kuuawa kwa wezi hao kwani walikuwa wakipoteza maisha yao.
Taarifa za kuuawa wezi hao zimetolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake na kubainisha kuwa wezi hao wameuawa baada ya kuiba pikipiki tatu aina Sanlg zenye Namba T.5888, T.363bfl na T.445cjt ambazo zimeokolewa baada ya wezi hao kuuawa.
Kwa upande wa waendesha bodaboda waliokusanyika kwenye Chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa ruvuma ilikohifadhiwa Miili ya wezi hao wamepongeza hatua ya kuuawa wezi hao kwani walikuwa wakiwaua waendesha Bodaboda na kupora Pikipiki zao.