Waandishi wa habari,mashabiki na wadau wa muziki jioni ya Dec 02 walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kwa Diamond Platnumz ambaye ameingia mchana wa leo na kutoa nafasi hiyo jioni.
Miongoni mwa vitu alivyovizungumza Diamond kwenye mkutano wake huu alisisitiza umoja kwa wasanii wa Tanzania ili kufikia nafasi ambazo nchi zingine kama Nigeria zimefika za kusimamisha wasanii wengi kwa pamoja.