Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA wilayani Ngara mkoani Kagera kimesema kimeshinda viti 7 vya Wenyeviti wa vijiji pamoja na vitongoji 76 tofauti na taarifa ya Msimamizi wa Uchaguzi huo, kuwa Chama hicho kimeshinda vijiji vitatu na vitongoji 43.
Katibu wa Chadema wilayani Ngara Bw Nestory Mashishanga amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Msimamizi Msaidiz wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani Ngara ,kueleza kuwaTakwimu alizokuwa nazo kufikia juzi Desemba 16,2014, CHADEMA kilikuwa na Vijiji vitatu na Vitongoji 43.

Amesema kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na uchaguzi uliofanyika jana Desemba 17,2014, katika vijiji 8 vilivyokuwa vimesalia pamoja na kijiji cha Mbuba kitakachofanya uchaguzi Jumapili ijayo baada ya kushindikana kufanyika Jumapili iliyopita.

Hapo jana Desemba 17,2014, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wilayani Ngara Bw Fred Kakuru amesema matokeo yaliyokuwa yamepatikana kufikia juzi Desemba 16,2014,yanaonesha kuwa Chama cha Mapinduzi –CCM kinaongoza kwa kushinda vijiji 61 na vitongoji 226, CHADEMA imepata vijiji vitatu na vitongoji 43 huku NCCR Mageuzi wakipata kijiji kimoja na kitongoji kimoja.


Chanzo:-Radio Kwizera FM-Ngara.

 
Top