Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Nchini Tanzania leo,June 20, 2016 wametumia mtindo mpya kueleza hisia zao baada ya kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge,mjini Dodoma wakiwa wamejifunika midomo kwa karatasi.
Hii ni wiki ya pili mfululizo Wabunge hao wamekuwa wakitoka Bungeni baada ya kutangaza kutohudhuria kikao cha Bunge kinachoongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi),Mhe. James Mbatia amesema wameamua kutumia mtindo huo mpya kwa sababu Bunge limekataa kuwasikiliza hoja zao.


Mbunge ,James Mbatia amesema wameanza kutoka kwa kufunga midomo na karatasi kuambia dunia kuwa bajeti imejaa ghiriba na udanganyifu mwingi kwa Watanzania.

Amesema watakwenda kuwaambia wananchi na hata kama mikutano imezuiwa, Rais John Magufuli asitegemee kwamba watanyamaza.

"Harakati hizi tulizianza tukiwa Chuo Kikuu na Dk Magufuli nilikuwa naye japo alikuwa mbele yangu. Dk Ackson alikuwa shule ya msingi na tangu wakati huo, harakati zinaendelea," amesema Mbatia.



 
Top