Katibu wa Chadema wa mkoa, Henry Kilewo 

Jumanne wiki hii, Rais John Magufuli alitegua mtego wa Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda kwa kumsimamisha kazi ukurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Kabwe kwa madai ya kusababisha hasara ya zaidi ya Sh3 bilioni.
Dar es Salaam. Uongozi wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam umesema mbali na kuadhibiwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, bado kuna siri kubwa ya mikataba mingi mibovu ambayo imeendelea kulindwa na viongozi wa Serikali.

Jumanne wiki hii, Rais John Magufuli alitegua mtego wa Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda kwa kumsimamisha kazi ukurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Kabwe kwa madai ya kusababisha hasara ya zaidi ya Sh3 bilioni.

Akizungumza jana Katibu wa Chadema wa mkoa huo, Henry Kilewo alisema: “Ukawa tuliwahi kueleza udhaifu wa mikataba iliyopo kwenye uongozi wa jiji, lakini hakuna kilichofanyika.’’

Kilewo alikosoa utaratibu wa kumuwajibisha mkurugenzi huyo.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema wa mkoa huo, Bernard Mwakyembe alisema uwajibishaji uliofanyika hautakuwa na tija endapo hatua hazitachukuliwa dhidi ya Kabwe. 

CREDIT: MWANANCHI
 
Top